Jumatano 3 Juni 2026 - 12:10
Kwa mnasaba wa kuadhimisha Idi Kubwa ya Mwenyezi Mungu; Ataba Tukufu ya Alawi yafanya hafla ya kupandisha bendera ya Ghadir

Hawza/ Ataba Tukufu ya Alawi imefanya hafla ya kupandisha bendera ya Ghadir katika viwanja na eneo la Haram Tukufu ya Amirul-Muuminin (as).

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ataba Tukufu ya Alawi ilifanya hafla ya kupandisha bendera ya Ghadir «مَن كُنتُ مَولاه فَهذا عَلیٌ مَولاه» katika viwanja na maeneo ya Haram Tukufu ya Amirul-Muuminin (as); hafla ambayo ni mwanzo wa shughuli za “Wiki Tukufu ya Ghadir” kwa mnasaba wa kuadhimisha “Idi Kubwa ya Mwenyezi Mungu”.

Hafla hii ilifanyika kwa ushiriki wa wageni wa Haram Tukufu ya Alawi, wakiwemo wawakilishi wa Mar'aji' wakuu wa Taqlid, wanazuoni, walimu na wanafunzi wa vyuo vya kidini, wasimamizi na wawakilishi wa Ataba Tukufu na maeneo matakatifu ya ziara, masheikh wa makabila, viongozi wa kijamii pamoja na wakurugenzi wa taasisi rasmi za mkoa wa Najaf Ashraf. Vilevile alihudhuria Sayyid Isa Al-Kharsan (msimamizi wa Ataba Tukufu ya Alawi), msaidizi wake, wajumbe wa bodi ya usimamizi, wakuu wa idara na wahudumu wa Haram Tukufu.

Hafla hiyo ilianza kwa kusomwa aya za Qur’ani Tukufu, kisha Haider Al-Isawi (mjumbe wa bodi ya usimamizi) aliwasilisha hotuba ya Sekretarieti ya Ataba, baadae, msimamizi wa Ataba Tukufu alipandisha bendera ya Ghadir juu ya kuba ya Haram Tukufu ya Amirul-Muuminin (as).

Sambamba na hatua hiyo, bendera tukufu za Ghadir zilipandishwa kwenye zaidi ya miji 150 katika maeneo mbalimbali ya Iraq na duniani kote, zikiwemo Ataba Tukufu, maeneo matukufu ya ziara pamoja na viwanja vikuu vya miji; hatua ambayo inadhihirisha maana ya Wilayah na uaminifu kwa Kiongozi wa wachamungu, Amirul-Muuminin (as).

Shughuli za “Wiki ya Kimataifa ya Ghadir” zilianza leo, Jumatatu tarehe kumi na tano Dhul-Hijjah mwaka 1447 Hijria, wiki hii inajumuisha programu za Qur’ani, kitamaduni na za kijamii, sherehe maalumu kwa wanawake, programu maalumu kwa watoto na vijana, maonesho ya turathi za kitamaduni na vitu vya thamani, pamoja na mipango ya kuimarisha mshikamano wa kijamii.

Programu hizi zinafanyika sambamba na utekelezaji wa miradi ya huduma na maandalizi kamili ya kuwapokea mazuwaru wanaoelekea Najaf Ashraf kwa ajili ya kuhuisha ziara ya mamilioni ya watu katika Idi Tukufu ya Ghadir.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha